Afrika Ya Mashariki

Afrika Ya Mashariki

Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
00:00
00:00

Resumen del episodio

Kwa miaka mingi, adhabu ya viboko imekuwa mojawapo ya njia zinazotumiwa na walimu kudhibiti nidhamu ya wanafunzi shuleni nchini Tanzania. Hata hivyo, matumizi yake yameendelea kuzua mjadala kutokana na madhara ya kimwili na kisaikolojia kwa watoto. Novemba 3, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi wa kihistoria wa kubatilisha vifungu vya kanuni zilizokuwa zikiruhusu adhabu ya viboko mashuleni, jambo lililo ibua mjadala nchini humo. Tunaangazia na kujiuliza Je, Tanzania iko tayari kujenga mfumo wa nidhamu usiotegemea nguvu za kimwili? Huku baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki zikifuta kitambo adhabu hiyo

Episodios

172-

Kufutwa kwa adhabu ya viboko shuleni nchini Tanzania

Kwa miaka mingi, adhabu ya viboko imekuwa mojawapo ya njia zinazotumiwa na walimu kudhibiti nidhamu ya wanafunzi shuleni nchini Tanzania. Hata hivyo, matumizi yake yameendelea kuzua mjadala kutokana na madhara ya kimwili na kisaikolojia kwa watoto. Novemba 3, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi wa kihistoria wa kubatilisha vifungu vya kanuni zilizokuwa zikiruhusu adhabu ya viboko mashuleni, jambo lililo ibua mjadala nchini humo. Tunaangazia na kujiuliza Je, Tanzania iko tayari kujenga mfumo wa nidhamu usiotegemea nguvu za kimwili? Huku baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki zikifuta kitambo adhabu hiyo

21 nov. 2026
171-

Makala: Hali ya usalama Beni, uwezo wa ADF na changamoto za serikali ya DRC

Mauaji ya raia, mashambulizi dhidi ya vijiji, utekaji nyara na uharibifu wa mali vimeendelea kuibua maswali kuhusu uwezo wa serikali ya DRC kuwalinda wananchi wake. Katika Makala ya Afrika Mashariki, hii leo tunaangazia nyuma ya mauaji ya ADF, nani anaendeleza vurugu mashariki mwa DRC?

14 nov. 2026
170-

Mauaji katika ndoa na migogoro ya kimahusiano Afrika Mashariki

Hii leo tunaangazia mauaji yanayotokana na migogoro ya kimahusiano, tukichunguza takwimu zilizopo, na sababu zinazochangia ukatili huo.

30 oct. 2026
169-

Teknolojia ya anga na matumaini mapya kwa jamii za bonde la Ziwa Victoria

Katika mwambao wa Ziwa Victoria, mamilioni ya wananchi wanategemea kilimo, uvuvi na ufugaji wa samaki kwa ajili ya chakula na kipato. Hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi, kutotabirika kwa hali ya hewa na changamoto za uzalishaji vinaendelea kuathiri maisha yao. Je, teknolojia za satelaiti zinaweza kumsaidia mkulima kujua wakati unaofaa kupanda, mvuvi kufanya maamuzi sahihi na mfugaji wa samaki kupunguza hasara? Kupitia mradi wa KijaniSpace unaotekelezwa Tanzania, Kenya na Uganda kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya, teknolojia za anga na taarifa za kidijitali zinatazamwa kama sehemu ya suluhisho la changamoto hizo. Karibu katika Makala ya Afrika Mashariki, hii leo tunaangazia namna ubunifu wa kiteknolojia unavyoweza kubadili maisha ya wananchi wanaoishi katika bonde la Ziwa Victoria.

24 oct. 2026
168-

Urembo kwa njia ya upasuaji

Karibu katika makala ya Afrika mashariki inayochunguza uhusiano kati ya urembo, kujiamini na shinikizo la kijamii. Tutaangazia simulizi za mwanawake aliyechagua kufanyiwa upasuaji wa urembo, pamoja na mitazamo ya wataalamu na wananchi.

17 oct. 2026